Yanga Kuwaongezea Mikataba Nyota Wake.

Klabu ya Yanga ipo kwnye mpango wa uongezea mkataba nyota wake wengine saba amba mikataba yao inakaribia kufika ukingoni.

Miongoni mwa nyota ambao wanakipiga ndani ya Yanga na mikataba yao inakaribia kuisha ni pamoja na:- Haruna Niyonzima, Mapinduzi Balama, Said Juma Makapu, Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Abdulaziz Makame na Deus Kaseke.

GSM imepanga kuwaongezea fasta mastaa hao ili kuwazuia Simba wasiwachukue kama ilivyokuwa kwa Bernard Morrison raia wa Ghana ambaye aliichezea Yanga kwa miezi sita, kisha akajiunga na Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Akizungumza jijini Dar, Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM na Makamu Mwenyekiti wa Usajili wa Yanga, Injinia Hersi Said, amesema kuwa zoezi hilo la kuwaongezea mikataba wachezaji wao wamepanga kulifanya kuwa endelevu.

Hersi amesema kuwa anaamini katika kikosi chao wapo baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao ipo mbioni kumalizika, hivyo kama wadhamini wamepanga kuhakikisha wanawabakisha kuendelea kukipiga Jangwani kwa lengo la kuiletea klabu mafanikio.

Aliongeza kuwa wachezaji hao watakaowabakisha ni wale wenye tija kwenye timu kwa kipindi chote walichoichezea Yanga bila ya kuangalia ukubwa wa jina lake.

“Huu mpango wa kuwaongezea mikataba tuliouanza tumepanga kuendelea nao siku za mbele ikiwa ni baada ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili beki wetu, Lamine Moro.

“Moro tumemuongezea mkataba baada ya kutambua mchango wake katika timu, hicho kigezo tulichokitumia kwake ndiyo tutakavyotumia kwa wachezaji wengine kuwaongezea mikataba.

“Tulianza kwa Moro, hivyo wachezaji wengine wanafuatia hivi sasa uongozi unapitia mkataba wa kila mchezaji kwa yule ambaye unakaribia kumalizika kwa kufuata vigezo vyetu, basi tutamuongezea mwingine,” alisema Hersi.

Ikumbukwe kuwa, GSM katika usajili wa dirisha kubwa msimu huu, ilihusika kwa kiasi kikubwa kushusha nyota wapya ndani ya Yanga.

Miongoni mwa nyota hao ni Carlos Carlinhos raia wa Angola, Michael Sarpong (Ghana), Yacouba Songne (Burkina Faso), Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ambao wote ni raia wa DR Congo.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

25 Komentara

    Habar njema kwa mashabik na wapenzi wajangwani kuwabakisha wachezaj muhimu ndani ya kikos cha wanajangwani hao

    Jibu

    Niswala zuri ikizingatiwa niwachezaji tegemezi wasije kufanya makosa wakawapoteza kama walivyo mpoteza morson wakati bado wanamuhitaji

    Jibu

    Gsm ameleta mapinduzi makubwa sana yanga na wachezaji wana hali ya kuitumikia klabu yanga wape salam

    Jibu

    Gud idea

    Jibu

    Yanga wafanye kweli wasije wakaleta lawama hapo baadae

    Jibu

    Safi sana wananchi

    Jibu

    inabidi yanga wachangamke kufanya ivyo ili wasije wakawapotea wachezaji waoo mahili

    Jibu

    Wamefanya vizuri sana kwa kuwaongezea mkataba maana Ni watu wa muhimu kwenye klabu

    Jibu

    Wamefanya jambo la msingi sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Ni vizuri sababu swala hili uwaongeza wachezaji motisha na Morali ya kujituma zaidi kwa ajili ya maslahi ya timu na maslahi binafsi

    Jibu

    Ni Jambo nzur kwa wan jangwani!!

    Jibu

    Yanga hawana jipya.leo tunasikia mikataba endelevu kesho tena tutasikia mambo mengine..wakae chini wajipange kama ndo hivyo kweli itakuwa mikataba endelevu.basi kila la kheri wana jangwani

    Jibu

    Vizuri Sana ilawafanye kweli hiyo mikataba isije badae kuleta mizozo kwenye timu watu wakanza kutafutana

    Jibu

    Maamuzi yao ni sahihi

    Jibu

    Jambo zuri

    Jibu

    Yanga oyeeeeee

    Jibu

    Kitendo cha yanga kuwaongezea mikataba wachezaji wake hii kinawafanya wajisajiliwe na timu nyingine ili kuimalisha kikosi na kuifanya timu iwe imara

    Jibu

    wazo zuri

    Jibu

    Ni vizuri sana jinsi gani yanga wameonesha bado wana umuhimu na wachezaji wao

    Jibu

    Yanga inafanya vizur

    Jibu

    Hongeren

    Jibu

    yanga wameonesha bado wana umuhimu na wachezaji wao

    Jibu

    Ni jambo nzur

    Jibu

    Habar njema kwa mashabik na wapenzi wajangwani kuwabakisha wachezaj muhimu ndani ya kikos cha wanajangwani hao

    Jibu

Acha ujumbe