Zlatko Krmpotić kwa sasa ndiye Kocha Mkuu wa Yanga ametua akitokea nchini Serbia kuchukua nafasi ya Mbelgiji, Luc Eymael aliyetimuliwa Julai 27.
Yanga imemchukua kocha huyo akitokea Polokwane City ya nchini Afrika Kusini huku akiwa amefundisha baadhi ya klabu kama APR (Rwanda), Zesco United (Zambia) na TP Mazembe (DR Congo).

Timu hiyo imemchukua kocha huyo baada ya Mrundi, Cedric Kaze aliyekuwa anafundisha Academy ya Barcelona kupata matatizo ya kifamilia.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema :- “Baada ya dili kufeli, haraka tukahamia kwa Zlatko ambaye yeye alikuwa chaguo letu la pili kati ya makocha hao walioleta CV zao Yanga, hivyo kamati ikachukua maamuzi ya kumpitisha Mserbia huyo kuja kuifundisha Yanga,

“Uzoefu wa Zlatko wa kufundisha timu za Afrika ndiyo umetushawishi sisi viongozi kumpa nafasi ya kuja kuifundisha Yanga, kwani aliwahi kuzifundisha klabu za TP Mazembe, Zesco na Polokwane, kocha huyo tumemuachia nafasi mbili za usajili za wachezaji wa kigeni ambazo kama akihitaji mchezaji wake atakayetaka kufanya naye kazi tumsajili,” amesema Hersi.
Amewahi kuwa kocha bora kule DR Congo msimu wa 2016-2017, msimu uliofuata pia akawa kocha bora kwenye Ligi ya Zambia akiwa na Klabu ya Zesco pia akawa kocha bora Afrika. Mwaka 2018 baada ya kutua Botswana kuinoa Jwaneng Galaxy aliibuka pia kocha bora wa msimu.

“Msaidizi ni Juma Mwambusi ambaye ni mzawa na ni pendekezo la kocha mpya kwamba alitaka kufanya kazi na mzawa.

“Pia, kocha wetu mpya wa makipa ni Niyonkuru (Vladimir) ambaye ni raia wa Burundi yupo tayari nchini kwa kufanya kazi yake hiyo, tumeliboresha benchi letu la ufundi kwa ajili ya kufi kia malengo yetu,” alisema Hersi.
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


Johnmary joel
Hongera zake kwa kuwa kocha mkuu wa yanga kila raheri katika mapambano#meridianbett
Dorophina
Kila lakheri zlatko katika utendaji wako wa kazi yanga wamekuamini ukafanye kweli
Devotha
Kila la kheri kwake akawajibike vema
rama
ngoja tuone uwezo wake yanga itabadilika
felister
namtakia mafanikio mema uenda akatufikisha mbali
Mwajumah
Kila la kheri kwake na namtakia mafanikio mema#Meridianbettz
Fatina mfingi
Kila kher kwake namtakia mafanikio mema na kujituma awapo kazin kwake!!
Caroline
Safi Sana Yanga
Ernest
Hakuna jinsi sasa ni kumwamini na kumsupport ili atimize majukumu yake kama kocha
Tatu
Tunasubili mabadiliko tu yanga
Povel
Hakun jinsi hapo wampe nafas tu hapo na wamtimizieh mahitaji anayoyatak iliawez kufany kaz kwa ueheredi hapo jangwani
Fatuma kasomo
Kazi kwao yanga
Mwanahamisi
Safi sana yanga
Lydia Emmanuel Magoti
Tunataka mahajabu uwanjani sio maneno tuuu ufanye kaz Sana kuipambania krabu yako nawamtimizie maitaji yake
Agness
Nihabari njema kwa wana yanga
Latifa juma mohamed
Kila la kheri ktk mapambano kocha mkuu wa yanga, tunahitaji uendeleze mapambano zaidi.
Sadick
Inadaiwa amekuwa hakai ktk timu moja kwa muda mrefu kutokana na matokeo mabaya tuone kama hapa atakaa muda mrefu #meridianbettz
aisha
Jitahidi baba sisi tunataka mabadiliko ya kweli
Nasra
Tunasubir mabadiliko
Amiri Kayera
Lakn bado ni kocha mzur
Rehema
Big up. Kwa Yanga Africa
farida ahmadi
Ngoja tujionee wenyewe mashabiki
neema hassan
Asante kwa taarfa
Rose kapinga
Kocha kama kocha hatar sana
Hidaya
Hawachelewi kumtimua na huyu
Hope mwaikuka
Haya karibu utopolo
Furahav
Haya tuone mabadiliko.
Amani
kumwamini na kumsupport ili atimize majukumu yake kama kocha katika timu yake ya uto
JULIANA
Tushawazoea amna jipya
Neema
Safiii sana Yanga
Sabrina
Yani daima Mbele nyuma mwiko
Samiah
Mmmmh😏😏😏
lombo
asante meridianbet kwa habar moto moto
Zeiyana
Yanga hawana mchezo mchezo kata mti panda mti hawataki machauzi
Leonard
Kocha mzuri atatufaa yanga
Issa
Kwa skwad hii bila kocha watakaa
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Ester jackson
Duuh nangoja kuona kivumbi cha yanga mana akiaribu tu tiketi ya ndege inamuhusu yanga hawataki mchezo
Theonestina
Mmmh
Sauda
Yuko vizuri, atatufaa wana Yanga
warda
Mmmmmmm Hakuna kitu hapo
magdalena
hapo naona hakuna jipya yanga wajipange sana
aisha
Kocha makini sana na kwa kikosi hiki patakuwa na ushindani
Shafii
Kwa CV alizokua nazo ninaimani atafanya makubwa ndani ya clubu ya yanga.
David Pere
Hakun jinsi hapo wampe nafas tu hapo na wamtimizieh mahitaji anayoyatak iliawez kufany kaz kwa ueheredi hapo jangwani
Gabriel
Zlatko Krmpotić n kocha mzur sana tena n kocha mzoef wa kimataifa nkubal sana 👍