Yilmaz Astaafu Timu ya Taifa.

Mchezaji mkongwe na nahodha wa timu ya Taifa ya Uturuki, Burak Yilmaz, ametangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo baada ya muda mrefu.

Yilmaz (miaka 36) amefikia hatua hiyo baada ya Uturuki kuambulia kipigo cha goli 3-1 kutoka kwa Ureno kwenye mchezo wa mtoano kuiwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia, 2022.

Kwenye mchezo huo, Burak alipachika goli 1 na kushindwa kufunga mkwaju wa penati wakati matokeo yakiwa ni 2-1 kabla ya Ureno kuongeza goli la 3 na kuimaliza safari ya Uturuki kwenye mashindano hayo.

Kwa Yilmaz, anaamini huu ni muda sahihi wa kukabidhi mikoba ya kuiongoza timu hiyo kwa wachezaji wengine akichagiza kuwa, timu hiyo inahitaji kufanyiwa mabadiliko makubwa na huu ndio muda wa kufanya hivyo. Anasisitiza kuwa, ataendelea kuwa sehemu ya mabadiliko hayo akiisaidia timu yake ya Taifa akiwa nje ya kikosi hicho.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe