Timu ya Zesco United ya Zambia imefanikiwa kubeba ubingwa wa Zambia Super League kwa mara ya nane sasa baada ya kupoteza ubingwa huo mwaka jana kwa Nkana.
Zesco United ilipata ushindi wa 2-0 katika mechi yao dhidi ya Napsa Stars hapo jana ili kujihakikishisa nafasi ya kubeba ubingwa huo kwa mara ya nane sasa.
Magoli ya Were na Kampamba ndio yaliyosaidia klabu hii ya Ndola kujipatia ushindi wake na kujinyakulia ubingwa huo wa Zambia.
Wenyeji wa mchezo huo, Zesco walitawala mchezo huo hususan dakika 20 za mwisho na wakaongeza ushindi wao kwa kufunga goli la pili kupitia Kampamba mnano dakika ya 80.
Kikosi hicho chenye maskani yake huko Ndola Zambia kiliibuka ushindi ubingwa kwa kufikisha alama ambazo hazitofikiwa na timu yoyote hata kama zitashinda mechi zote mbili zilizobaki.
SHINDA TSH 150,000,000/=
Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑



magdalena
Hongera yao
Hope mwaikuka
Congrats to them