Zinedine Zidane na Rekodi Mbovu ya Namna Alivyostaafu

Ili kushinda vita ni lazima ujue muda gani upambane, muda gani ujifiche na muda gani ukimbie, bila shaka unamkumbuka Zidane kwenye ubora wake, alikua ni Goliath wa soka, lakini mtoto mdogo tu Marco Materrazi alitumia akili ndogo kumshinda

Katikati ya ubora na ufundi mkubwa na kuibeba Ufaransa mgongoni mwake, ila Zidane akaja kuwa adui mkubwa na kusemwa sana na Wafaransa, Zizzou alimuuliza Materrazi “Unahitaji jezi yangu?” ila Materrazi alimjibu “Namtaka Dada yako”, hapo Zizzou aligeuka kuwa Mwarabu halisi, akala umeme fainali world cup 2006 pale German

Yupo wapi yule Daudi aliemwangusha Binadamu aliesimama kwenye ukumbi mmoja pale Basel Uswizi, 2003 akibeba tuzo ya mchezaji bora wa dunia, alikua ni General wa soka na Maestro uzawa wa Algeria, haikuwa tuzo yake ya mara ya kwanza au ya pili bali ni ya tatu

Pengine labda Daudi hakujua kuwa alimuangusha Goliath, aliefanya makubwa kwenye tuzo kabla ya ujio wa Ronaldo na Messi, labda amesahau kuwa baada ya kichwa cha Angelos Charisteas kilichowatoa France robo fainali ya Euro 2004, Zizzou alitangaza kustaafu

Lakini tangazo lake lilikataliwa na Wafaransa wote, Kocha Raymond Domenech na wanasiasa nguli kama Nicolaus Sarkozy, kila mtu alitaka arejee uwanjani, akakubali kuvaa upya viatu vyake, kuvaa upya kitambaa chake na jezi yake namba 10 ya Les Blues, kwa ajili ya kombe la dunia 2006

Alirejea wakati ambao timu ilimuhitaji zaidi, wakahitaji pass zake, swashbuckling, tantalizing football na Panenka zake, aliibeba timu mgongoni mwake mpaka zile fainali pale Ujeruman, hakuna aliejua kuwa mwisho wake utakua mbaya zaidi ya ule wa 2004

Nakumbuka pia Goliath alitangaza kustaafu soka la klabu Mei 7 pale Bernabeu, uwanja ulijaa nembo ya ‘Zidane 5’, alipiga goli lake la mwisho kwenye ile sare ya 3-3 dhidi ya Villareal mbele ya Alfredo di Stefano, ilikua cross ya Beckham, baadae alirejea kuwaaga na machozi yakimtoka sana

44 Komentara

    Hii ni mpya kwangu mko vizuri kwa habari

    Jibu

    Kwake anaona sawa mana kila mmoja anautaratibu wake wa kustaafu ila kwa wengine wanaona mbaya na kwasasa ameonyesha kuwa yeye ni kocha mzuri sana

    Jibu

    Habari nzuri sana

    Jibu

    Zizzou zidane maestro kipenz cha Ferguson

    Jibu

    Zinedine zedani zizzuu mchezaji aliyeacha historia vichwani mwa wapenda soko hakika alifanya mengi ya kuvutia akiwa uwanjani

    Jibu

    Alochokifanya Zinedine sio kibaya huo ni uamuzi wake na hakuna mtu wakuweza kumzuia kustaafu japo inasemekana ana rekod mbovu

    Jibu

    Vizur

    Jibu

    Hii ni habari mzuri sn

    Jibu

    Nakala nzuri hii inatukumbusha mbali

    Jibu

    Asante kwa habari#meridianbettz

    Jibu

    Zidane atakumbukwa na wengi ktk ulimwengu wa soka

    Jibu

    Nakala hii nzuri inanikumbusha mbali

    Jibu

    Habari nzuli kwetu mashabiki #meridianbettz

    Jibu

    zidane atakumbukwa daima

    Jibu

    Kweli ukitaka kushinda lazima upambane

    Jibu

    Kwa uchezaji alio kua nao ni wakiwango kikubwa sana.na kustaafu kwake soka aliona ni sawa na tunajua uwezi kumlidhisha kila mtu umapo fanya jambo lako,ila yeye zidan anatuonesha akua bora tu kwenye uchezaji bal ata kua kocha bado anaonesha kua ni bora zaid

    Jibu

    Kumbe ndo ilvyo

    Jibu

    Nilikuwa siyajui haya kwa kusoma makala hii nimeyajuwa sasa.

    Jibu

    Zidane tutamkubuka sana maana amefanya mengi

    Jibu

    Asanteni kwa habari

    Jibu

    meridian mko vizuri kwa kutukumbusha mambo mbali mbali ya sasa na ya zamani

    Jibu

    Habari nzuri sana

    Jibu

    Tnx meridian kwa update

    Jibu

    Namkumbuka kwa jina mojaa kali sana Zizzou

    Jibu

    True Legend of our time#meridianbettz

    Jibu

    True Legend of our time now nikocha Bora barani ulaya big up zizzou#meridianbettz

    Jibu

    Habari nzuri sana hz

    Jibu

    Habari njema Sana hizi

    Jibu

    huyu ndiye fundi ambaye alikua na vitu vyote, maana anachezea mpira na anafunga pia

    Jibu

    Kiungo fundi! Aliyestaff soka akiwa na uwezo mkubwa

    Jibu

    huyu katika ujana wake hakuwa mchezaji hatari lakini uzeewake alikuwa moto

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Zidane atakumbukwa daima

    Jibu

    Kiungo mshambuliaji bora

    Jibu

    Zidane ni kocha hodari

    Jibu

    gud newz asante

    Jibu

    Alikua mchezaji mkubwa Sana ulimwenguni ila kwa tukio lile Lilikua ni utovu wa kinidham

    Jibu

    Makara mazuri sana

    Jibu

    Zidane ninmchezaji Bora atazid kukumbukwa licha ya matatzo yake

    Jibu

    Zidane ni mchezaji mzuri Sana atakumbukwa.

    Jibu

    Zidanne aliacha historia nzuri Sana katika mpira na atakumbukwa sana

    Jibu

    Zidane.long tym sana

    Jibu

    Angelos Charisteas kile kichwa alijirusha coz aliamua kumchafulia mkongwe huyo historia

    Jibu

    Zizzou fundiiiii sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.