Benfica Wapigwa Mawe na Mashabiki

Wachezaji wawili wa mabingwa wa ligi kuu ya Ureno, klabu ya Benfica wameumia baada ya basi la timu hiyo kushambuliwa kwa kupigwa mawe na mashabiki wa timu hiyo.

Tukio hilo linalolaaniwa na wadau mbalimbali wa soka dunia kote, limetokea siku ya alhamisi ikiwa ni baada ya Benfica kucheza mechi yao ya kwanza kabisa kutokea kwenye likizo ya dharula ya ugonjwa wa Corona.

Mashabiki hao walifanya tukio hilo kama ishara ya kuonesha hasira zao baada ya Benfica kutoa suluhu ya bila kufungana na timu inayoshika nafasi za chini kabisa katika msimamo wa ligi hiyo, Tondela.

Matokeo hayo yanawafanya Benfica wabaki nafasi ya pili na alama zao 60 ambazo ni sawa na zile za Porto wanaoongoza msimamo huo, lakini kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Pamoja na kwamba ligi hiyo inaendelea bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na janga la Corona, mashabiki hao wa Benfica walizingira uwanja wa timu hiyo ili kuisapoti timu yao hiyo.

Mashabiki wa timu hiyo walilivamia basi hilo kulipiga mawe hali iliyopelekea kuvunja vioo vya basi hilo na kujeruhi wachezaji wawili wa timu hiyo, Julian Weigl na Andrija Zivkovic ambao wamewahishwa hospitali ya Hospital da Luz iliyopo ndani ya jiji la Lisbon.

44 Komentara

    Dah!pole kwao

    Jibu

    Kweli mashabiki sio kwa kuipenda timu yao hivyo kisa kuzuiwa kuingia uwanjani wameamua kuwashambulia inabidi wapewe elimu kuhusiana na kutohudhuria kushangilia timu zao kutokana na ugonjwa huu wa corona

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Daah ni tukio mbaya sana mashabiki ni vyema kudhibiti hasira zetu pole kwa majeruhi na timu nzima kwa ujumla

    Jibu

    Duuh hatari Sana pole zao

    Jibu

    Duuh maskini Benifica ni kweli mashabiki wanahasira lakini hawakutakiwa kufanya hivo kwani mpira huchezwa uwanjani na lolote linaweza kutokea sio makosa yao huenda wao walijipanga vizuri lakini wapinzani wao nao walikuwa vizuri zaidi yao ndio kilichosababisha suluhu

    Jibu

    Mmmh inasikitisha kwa kweli.pole yao

    Jibu

    Aisee pole sn

    Jibu

    Siku zote timu ikifungwa wanaoumia sana ni mashabiki,kwa tukio hilo walionyesha hisia zao

    Jibu

    Duuuh..pole yao

    Jibu

    Hasira hasara Sasa wameumiza wachezaji wanategemea nini zaidi ya kufungwa tu

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Too much fan imotions

    Jibu

    Siku zote timu ikifungwa wanao umia Sana ni mashabiki kwa tukio Hilo wameonyesha isia zao

    Jibu

    sad news

    Jibu

    Duuh polen sana#meridianbettz

    Jibu

    Jaman mashabiki wanatakiwa wawe na subra tunajua kama timu yao wanaipenda wajipe muda kwanza ili janga la corona lipite maana ata hao wachezaji pia wanaipenda wakiwa uwanjan na mashabiki pia wawepo ili wawape molali ya kucheza na kuipatia ushindi timu yao

    Jibu

    Jamani uongozi unatakiwa uwachukulie hatua hao mashabiki ili iwe fundisho bila ivo sikunyingine wanaweza wakaleta madhara zaidi.

    Jibu

    Sorry for them

    Jibu

    Pole sana benfica vipi tuambieni hakuna iliyeumia

    Jibu

    Pole sana kwa wachezaji wa benfica

    Jibu

    poleni sana kwa majanga

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Habari mbaya pole yao

    Jibu

    Hii Kali, Vyombo vya usalama vinahitajika kuwapa support wachezaji siku hizi wakiwa kwenye usafiri kabla na baada ya mechi

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Duu.!kumbe nako ulaya Kuna mashabiki vichaa…Kama bongo.

    Jibu

    hii ni picha mbaya

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Da kweli mpira umekuwa kama vita

    Jibu

    Hii ni picha mbaya sana

    Jibu

    polen sana watu hawatak masihal

    Jibu

    Sio poa kabisa

    Jibu

    Duh nihabali ya kusikitisha sana

    Jibu

    Wanabolonga Sana tatizo asahv

    Jibu

    Jamani pole yao.

    Jibu

    Hao mashabiki wamwfanya vibaya Sana kuwapoga nawe wachezaji wao

    Jibu

    Duh habari za kuhuzunishaaa Sana

    Jibu

    So sadπŸ™πŸΌπŸ™πŸΌπŸ™πŸΌ

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Ivi vitendo vinabidi kukemewa si vya kiungwana kabisa

    Jibu

    Day pole sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.