UEFA Yasitisha Mapendekezo Yake Mapya

Shirikisho la mpira wa barani ulaya UEFA wamesitisha mapendekezo yao ambayo yalipanga kuongeza wigo wa timu shiriki kwenye mashindano ya klabu bingwa barani ulaya ambapo timu ambazo zinahistoria nzuri kwenye mashindano hata kama hazitafanikiwa kufuzu.

Mapendekezo mapya ya UEFA yaliowekwa mezani yalikuwa yanaruhusu timu ambazo ziliwai kufanya vizuri kwenye mashindano hayo, kuweza kushiriki mashindano hayo hata kama hazikufanikiwa kumaliza nafasi ambazo zisingiweza kufuzu mashindano hayo.

UEFA

Kwa mfano, ikiwa klabu ya Manchester United ikimaliza nafasi ya sita nyuma ya west ham united ambayo ilishika nafasi ya tano, kutokana na Man Utd kufanya vizuri kwenye mashindano hayo kwenye misimu mitano iliyopita, basi atafuzu mashindano hayo na kushiriki.

Ingawa, taarifa zinasema kuwa mapendekezo hayo yameondolewa, na klabu hazitapata nafasi hiyo ya kuweza kupita kwa mgongo wa upendeleo wa matokeo ya nyuma.

Mapendekezo hayo yamekuja baada ya UEFA kutaka kuongeza idadi ya timu kutoka 32 hadi timu 36, awali kulikuwa na timu 32 ambazo zinawekwa kwenye makundi manne huku wakicheza michezo 6 kila mmoja, lakini mapendekezo mapya kungekuwa na timu 36 na kila timu ingecheza michezo angalau 10 ili kuweza kufuzu 16 bora.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe