Mshambuliaji nyota wa klabu ya Juventus Paulo Dybala amichagua klabu ya Atletico Madrid kama klabu ambayo anahitaji kwenda kucheza baada ya kuondoka kwenye viunga vya Turin mwisho wa msimu kama mchezaji huru.
Mazungumzo kati ya Juventus na Paulo Dybala yameshindakana kutokana na kushindwana kwenye maswala ya makubaliano ya mshahara, anajiandaa kuacha kitambaa cha unahodha na jezi namba 10 pindi tu msimu utakaopisha.
Nafasi ya Paulo Dybala imekuwa shakani tokea kusajiriwa kwa Dusan Vlahovic ambaye ametokea kwenye klabu ya Fiorentina kwenye dirisha la usajiri la mwezi january, japokuwa Dybala bado yuko kwenye kiwango kizuri msimu huu huku akifanikiwa kufunga magoli 13 na kusaidia 6 kwenye michezo 29 aliyocheza.
Atletico Madrid wapo kwenye rada ya kuhitaji saini ya Martinez lakini hawako tayari kulipa €70million kama ada ya usajiri ya kumuondoa kwenye dimba la San Siro, huku mwaka 2018 alishafanyiwa mpaka vipomo vya afya pia aliondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ili kujiunga na Atletico lakini ilishindikana.
Atletico Madrid kumkosa Martinez kunatoa wigo wa kuweza kumpata Paulo Dybala pasipo ghalama kubwa kwa Diego Simeone ambaye amepanga kuingia sokoni ili kuweza kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.