Mchezaji wa FC Bayern Munich na timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane amejumuishwa kwenye kikosi cha Senegal cha Aliou Cisse kitakachoenda Qatar kwaajili ya Kombe la Dunia linalotarajiwa kuanza mwezi huu licha ya majeruhi.

 

Mane Ajumuishwa Kwenye Kikosi Cha Senegal

Sadio Mane alipata majeraha katika mchezo wao waliokuwa wakicheza dhidi ya Werder Bremen waliposhinda mabao 6-1 na mchezaji huyo kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kutoka uwanjani.

Jarida la Lequipe lilitoa taarifa mchezaji huyo ambaye ni mshindi wa Afcon Barani Afrika hatashiriki Fainali za Kombe la Dunia kutokana na kupata majeraha. Lakini sasa kocha wa timu hiyo Aliou ametoa jeshi lake na kumjuisha Sadio Mane.

Mane Ajumuishwa Kwenye Kikosi Cha Senegal

Ikumbukwe tu siku za hivi karibuni mchezaji huyo alishikilia nafasi ya pili ya mchezaji bora Duniani kwenye tuzo za Ballon d’Or baada ya Karim Benzema wa Ufaransa na Madrid kuchukua tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.

Pia Mane alipewa tuzo ya mchezaji anayejitoa sana kwenye jamii kutokana na mchango wake alionao kwenye jamii yake ya huko Senegal kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kujenga misikiti na hospitali na shule.

Mane Ajumuishwa Kwenye Kikosi Cha Senegal

Mchezaji wa Monaco ambaye pia hakujumuishwa kwenye kikosi cha awali Krepin Diata naye amejumuishwa kwenye kikosi kipya ambacho kimetoka leo.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa