Kinda wa klabu ya Manchester United Alejandro Garnacho ameweka rekodi katika mchezo wa jana klabu yake ilipokua nyumbani dhidi ya Aston Villa katika dimba la Old Trafford katika kombe la Carabao Cup.

Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Aston Villa wikiendi iliyomalizka klabu ya Manchester United jana waliwakaribisha Aston Villa katika Dimba la Old Trafford, Lakini wakati huu Mnachester United walifanikiwa kulipiza kisasi na kushinda kwa mabao manne kwa mawili.garnachoManchester United jana walitoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda mabao manne kwa mawili huku magoli ya klabu hiyo yakifungwa na Anthony Martial, Marcus Rashford, Bruno Fernandes na Scott Mctominay huku magoli mawili ya Aston Villa yakifungwa na Ollie Watkins na Leon Bailey.

Lakini kiwango kikubwa alichokionesha kinda wa kimataifa wa Argentina Alejandro Garnacho katika mchezo wa jana kimefanya watu kuendelea kubaki midomo wazi, Hii imetokana na kind huyo alietokea nje na kuingizwa kupiga pasi mbili za mabao katika mchezo huo.garnacho Kijana huyo mwenye miaka 18 amekua kwenye kiwango bora kwasasa kila anapopata nafasi ya kucheza ameingia kwenye vitabu vya historia ndani ya klabu hiyo, baada ya kuweka rekodi kama mchezaji mdogo zaidi kupiga pasi mbili za mabao katika mchezo mmoja klabuni hapo akiwa na miaka 18 na siku 133 tu.

Alejandro Garnacho anazungumzwa kama miongoni vijana wenye vipaji vya hali ya juu kwasasa na wengi wakimuona kama mchezaji atakaekuja kufanikiwa siku za mbeleni kama atakiendeleza hichi ambacho anakifanya kwasasa.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa