Kinda wa Manchester United Alejandro Garnacho amewacha watu midomo wazi, baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika katika mchezo wa Uefa Europa League uliopigwa katika dimba la Old Trafford usiku wa jana.garnachoKinda huyo mwenye kipaji kikubwa raia wa Argentina alionesha uwezo mkubwa katika mchezo huo ambapo Manchester United walipata ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya klabu ya Sherrif.

Licha ya umri wake mdogo wa miaka 18 ila ameonesha ubora wa hali ya juu katika mchezo jambo lililowafanya watu wengi kuamini kama ataendelea hivi basi atakua mchezaji bora siku za mbeleni.

Kocha wa klabu hiyo pia amezungumzia uwezo mkubwa aliouonesha Garnacho huyo katika mchezo huo na kuonesha kuvutiwa na mchezaji huyo kutokana na kiwango alichoonesha katika mchezo huo.garnachoTen akizungumzia uwezo aliounesha Garnacho katika mchezo wa jana na kusema hakuvutiwa na uwezo wa kinda huyo msimu ulipoanza lakini siku za karibuni ndio maana alimuanzisha katika mchezo wa jana.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa