Messi Dhidi ya Modric Nani Kucheka leo?

Timu ya taifa ya Argentina itakua uwanjani leo kukipiga na timu ya taifa ya Croatia kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la dunia, Huku watu wengi wakisubiri kati ya Lionel Messi nahodha wa Argentina na Luca Modric nahodha wa Croatia nani atafurahi mwezake akilia.

Mchezo huu utakaopigwa majira ya saa nne kamili usiku unachukuliwa pia kama mchezo wa kisasi kwani timu ya taifa ya Argentina ilikumbana na kichapo cha mabao matatu kwa bila dhidi ya Croatia kwenye mchezo wa makundi kombe la dunia 2018.messiLionel Messi ana jukumu kubwa la kuivusha timu ya taifa ya Argentina na kuipelekea fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili baada ya kufanya hivo mwaka 2014 na kukosa kombe hilo, Lakini mwaka huu timu hiyo inaonekana kua imara na bora zaidi kiujumla hivo kuwapa matumaini wengi wakiamini staa huyo anaweza kubeba kombe hilo.

Timu hizi zote zinaenda kucheza mchezo wa nusu fainali leo zikiwa zimefuzu kwa mikwaju ya penati katika michezo yao ya robo fainali baada ya mshindi kushindwa kupatikana katika dakika 120. Argentina dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi, Huku Croatia wao wakiwatupa nje Brazil kwa mikwaju ya penati.

Luca Modric yeye kama nahodha na jeshi lake wana nafasi kubwa ya kurudia historia kama ambavyo walifanya mwaka 2018 kwa kutinga fainali ya kombe la dunia, Timu hiyo imeonekana kua bora licha ya kutopewa nafasi kubwa wakati michuano inaanza lakini mpaka sasa wanashangaza watu kutokana na ubora wao.messiLionel Messi na Luca Modric wote wakiw manahodha wa timu zao za taifa kila mmoja ana nafasi ya kuweza kuhakikisha timu yake inatinga fainali ya michuano hiyo usiku wa leo katika mtanange wa nusu fainali kati ya timu ya taifa ya Argentina dhidi ya timu ya taifa ya Croatia.

Acha ujumbe