Chelsea Wamvuta Carney Chukwuemeka Kutoka Aston Villa

Klabu ya Chelsea imethibitisha kumsajiri mchezaji kinda kutoka klabu ya Aston Villa Carney Chukwuemeka ambaye pia ni mchezaji wa timu ya vijana chini ya miaka 19 ya Uingereza.

Carney Chukwuemeka amesaini kandarasi ya miaka sita ya kuwepo darajani. Kinda huyo mwenye miaka 18 alikuwepo kwenye kikosi kilichoshinda ubingwa wa Ulaya chini ya miaka 19 cha uingereza dhidi ya Israel huku yeye akiwa moja wa wachezaji waliofunga goli kwenye mchezo huo.

Carney mkataba wake na klabu ya Aston Villa ulikuwa unafikia tamati majira haya ya kiangazi na klabu ilipohitaji kumuongezea mkataba ili aweze kusalia kwenye kikosi cha Steven Gerrard aligoma na kuomba kuondoka.

“Imekuwa ni ngumu lakini sikuweza kuitoa chelsea kwenye akili yangu kwa siku kadhaa ila nina furaha na kuweza kumaliza hili.

“Nina furaha na nina shauku ya ya kujumuika na timu uwanjani, na kukutana na wachezaji wote na kuajaribu kushinda michezo na vikombe nikiwa na Chelsea.” Alisema Carney Chukwuemeka

 

 

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.