Vieira: Zaha(30) Atasalia Palace

Kocha wa timu ya Crystal Palace Patrick Vieira amesema kuwa mchezaji wake anayecheza katika timu  ya Taifa ya Ivory Coast na timu ya Crystal Palace haendi popote atabaki kukitumikia kikosi hicho baada ya dirisha hili la usajili.

Vieira: Zaha Atasalia Palace

Vieira anasema” Ninafanya kazi naye kila siku na hakuna kitu kitaingia akilini mwangu kwamba kitu kama (Zaha kuondoka kitatokea)

Hakuishia hapo  pia aliongeza kwa kusema kuwa kitu pekee anachoonyesha ni ushindani uwanjani, kufanya vizuri kwa klabu hii ya soka ambayo anaipenda sana. Patrick  Vieira ambaye ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu  aliichukua timu hii msimu jana ambayo ilikuwa chini ya kocha mkuu Roy Hodgson.

Vieira: Zaha Atasalia Palace

Willfred Zaha ambaye ni nyota wa timu hiyo amekuwa na kiwango kizuri sana msimu huu  hivyo kufanya kuwa na tetesi za yeye kutakiwa na timu mbalimbali ikiwepo Chelsea. Zaha  amekuwa akitoa mchango mkubwa sana katika timu yake hata ujio wa Vieira umemfanya aimarike lakini pia takribani kikosi kizima kimekuwa na ubora mzuri ambao unaleta ushindani kwa vilabu vikubwa na hata vilabu vya madaraja yao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.