Manchester United Yamsajiri Martin Dubravka

Klabu ya Manchester United Imethibitisha kumsajiri mlinda mlango wa klabu ya Newcastle United Martin Dubravka kwa mkopo wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengere cha kuweza kumsajiri moja kwa moja.

Martin Dubravka anaenda kuchukua nafasi ya mlinda mlango wa klabu ya Manchester United Dean Henderson ambaye alijiunga naklabu ya Nottingham Forest kwa mkopo mapema tu dirisha lilipofunguliwa kwenye majira haya ya kiangazi.

Manchester United baada kuoandoka Dean Henderson kwenye safu ya walinda mlango kulibakiwa na walinda milango wawili kwenye kikosi cha kwanza ambao ni David de Gea na Tom Heaton na kuhitaji kuongeza nguvu kwenye upande wa walinda mlango.

“Akili yangu kwa sasa ni kuisaidia Manchester United, na tutaangalia nini kitatokea mbeleni baada ya kutoa kila kitu kwenye msimu huu.” Nina furaha kuwa hapa. Alisema Martin Dubravka

Martin Dubravka ameichezea klabu ya Newcastle United michezo 130, kwenye kipindi chote alichokuwepo kwenye klabu hiyo, na kuwa mmoja wa magolikipa bora kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.