Pep Guardiola Aitaka City kujiimarisha Licha ya Ushindi.

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema timu yake inapaswa kujiimarisha zaidi ya kuifunga klabu ya Manchester United mabao sita kwa matatu katika mchezo wa ligi ya kuu ya Uingereza uliopigwa katila dimba la Etihad.

pep guardiolaPep Guardiola na vijana wake walifanikiwa kuifunga United kipigo cha fedheha cha mabao sita kwa matatu huku Earling haaland pamoja Phil Foden wakifanikiwa kufunga magoli matatu kila mmoja katia mchezo huo.

Licha ya ushindi huo kocha huyo amesisitiza timu yake inahitaji kujiboresha zaidi kuelekea michezo ijayo ya klabu hiyo baada ya kupaya matokeo mazuri leo dhidi ya mahasimu wake katika jiji la Manchester.

Pep Guardiola pia hakuacha kusifu ubora wa wachezaji wake haswa kipindi cha kwanza cha mchezo walipoonesha ukatili zaidi wanapokua na mpira na kutengeneza nafasi za mabao na kuweza kuondoka na uongozi wa goli nne kwa bila.

pep guardiolaKocha huyo pia alisifu kiwango cha United katika kipindi cha pili cha mchezo baada ya klabu hiyo kupata mabao matatu huku City wakipata mabao mawili na kusema walicheza vizuri zaidi kipindi cha pili kuliko wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.