Pep Guardiola Amtakia Kheri Alonso.

Pep Guardiola kocha wa klabu ya Manchester City amemtakia kila la kheiri kiungo wa zamani wa klabu ya Bayern Munich,Real Madrid, pamoja na Liverpool katika najukumu yake mapya kama kocha mkuu wa Bayern Leverkusen.

Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania alichaguliwa kua kocha mkuu wa klabu ya Bayern Leverkusen siku ya jumatano baada ya aliekua kocha mkuu wa timu hiyo Gerardo Seoane kufukuzwa kazi katika klabu hiyo.pep guardiola Alonso kabla ya kupata nafasi hiyo katika klabu ya Bayern Leverkusen amepita vilabu tofauti baada ya kustaafu soka mwaka 2017 kama timu ya Real Madrid chini ya miaka 14 kabla ya kujiunga kuifundisha timu yake ya utotoni ya Real Sociedad B.

Xabi Alonso na Pep Guardiola wote walitambulika kama viungo mahiri wakati wakicheza soka japo walipishana vipindi na wote wakiitumikia timu ya taifa ya Hispania.

“Alikua kiungo mkabaji wa kipekee, na unapokua kiungo mkabaji wa kipekee lazima uuelewe mchezo, Anasoma kikamilifu, na ni mtu mzuri wa kupendeza”Alisema Pep.pep guardiolaAkizungumza kwenye mkutano wa wanahabari leo Pep Guardiola alituma salamu za pongezi na kumtakia kheri kiungo huyo ambaye ameshawahi kumfundisha katika klabu ya Fc Bayern Munich.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.