Yanga Kutua Sudan Kimafia Jumamosi

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Shaban Kamwe alisema kila kitu juu ya mipango ya safari hiyo ipo tayari na watashuka kama majasusi kwenye ardhi ya Sudan na wanakwenda wakiwa na wachezaji wao wote muhimu.

Kamwe alisema, hakuna mchezaji hata mmoja ambaye atakosekana kwenye mchezo huo baada ya maandalizi yote kukamilika na watakwenda wakiwa na nguvu na ari moja ya kutaka kushinda na kuwaondoka wasudan.

“Tunakwenda Sudan kwa staili ya kijeshi, yaani ni kusaka kuandika historia ya kuwatoa Hilal wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani. Kila Mwananchi anataka kuona hilo likitokea na ninachoweza kusema kinakwenda kutokea.

“Timu itaingia Sudan saa sita mchana wachezaji watapumzika kidogo na watafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuingia uwanjani kwa mchezo huo,” alisema.

Yanga wanahitaji ushindi wa bao 1-0 au sare ya mabao zaidi ya moja ili waweze kuvuka kwenda kwenye hatua inayofuata ambayo ni makundi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.