IKIWA ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuingia kwenye Kombe la Dunia kupitia timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17, Serengeti wamefanikiwa kutnga hatua ya robo fainali.
Mchezo wa jana Oktoba 18 ambao ulikuwa ni watatu kwa Tanzania imeambulia sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Canada.
Kwenye mchezo huo ni Canada walianza kupata bao la kuongoza ilikuwa dakika ya 14 kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Amanda Allen na baadae mlinzi wa Tanzania Veronica Mapunda akasawazisha dakika ya 35.
Tanzania Inatinga hatua ya robo fainali ikiwa na pointi 4 kwa kuwa ilipata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Ufaransa na ilipoteza mchezo mbele Japan kwa kufungwa mabao 4-0.
Sasa watakuwa na kibarua cha kukutana na Colombia kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.

