Polisi Wapata Ushindi wa Kwanza Ligi Kuu

HATIMAE Polisi Tanzania wamepata ushindi wa kwanza tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu baada ya kuwafunga Namungo bao 1-0.

Mchezo huo ulipigwa jana jumatano kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya huku bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Rajabu Athuman dakika ya 40.

Ushindi huo umekuja baada ya kumsimamisha kocha Mkuu, Joslin Sharif na kikosi hicho kuwa chini ya John Tamba.

Akizungumza siri ya mafanikio hayo, Tamba amesema kuwa aliwajenga kiakili kwenda kupambana na kuhakikisha matokeo yanapatikana kwenye mchezo huo.

“Tunashukuru kupata pointi tatu hizi za kwanza tangu tuanze ligi kuu kwa msimu huu, zilikuwa ni muhimu kwa upande wetu kutokana na hali ilivyokuwa.

“Siri ya mafanikio niliwajenga kiakili kwamba twende tukashambulie ili tupate goli la kuongoza lakini tuzuie pia kwani mchezo uliopita safu ya ulinzi iliruhusu mabao mengi kipindi cha pili.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.