Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Poland na klabu ya Fc Barcelona Roberto Lewandowski amefanikiwa kufunga bao lake la kanza kwenye michuano ya kombe la dunia leo dhidi ya timu ya taifa ya Saudia Arabia.
Timu ya taifa ya Poland imefanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Saudia Arabia katika mchezo uliopigwa katika dimba la Education City ambapo staa wa timu hiyo alifanikiwa kufunga moja katika mchezo huo.
Lewandowski amefunga bao lake la kwanza la michuano ya kombe la dunia ikiwa ni furaha kubwa kwake kwani siku kadhaa nyuma alieleza namna ambavyo anatamani kufunga kwenye michuano hiyo mikubwa zaidi duniani kwenye ngazi ya mpira.
Timu ya taifa taifa ya Poland sasa imefanikiwa kukwea hadi kileleni kwenye msimamo wa kundi C ambapo wamefikisha alama tatu na kuwashusha Saudia Arabia ambao walikua wanaongoza kwa alama tatu baada ya kuifunga timu ya taifa ya Argentina.
Roberto Lewandowski amekua na mchezo mzuri sana dhidi ya Saudia Arabia kwani amehusika katika magoli mawili baada ya kupiga pasi ya bao la kwanza kwa Piotr Zielenski na kuhitimisha ushindi baada ya kufunga bao la pili.
Poland sasa wamejitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu kwenye hatau ya 16 bora baada ya kupata ushindi katika mchezo wa leo lakini bado watahitaji mchezo wa mwisho dhidi ya timu ya taifa ya Argentina kupata matokeo mazuri ili waweze kufuzu.

Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

