Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Poland na klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania Roberto Lewandowski anawaza kufunga bao lake la michuano ya kombe la dunia mwaka huu yanayofanyika nchini Qatar.

Mshambuliaji Roberto Lewandowski anasalia nado kua mshambuliaji hatari licha ya klabu yake kutokufanya vizuri lakini mpaka sasa msimu kashaweka kambani mabao 18 akiwa nyuma ya Earling Haaland mwenye mabao 23, na  Kylian Mbappe mwenye mabao 19.lewandowskiMshambuliaji huyo mpaka sasa maefanikiwa kua mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo akiwa na mabao 76 kwenye michezo 134 huku akiwa bado hajafanikiwa kufumania nyavu kwenye michuano ya kombe la dunia.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Bayern Munich ana ndoto za kuifungia nchi yake bao kwenye michuanbo ya kombe la dunia huku wakitaka kuepuka makosa ya mwaka 2018 pale ambapo walishindwa kuvuka hatua ya makundi kwenye michuano hiyo.lewandowskiPoland walishindwa kufuzu michuano hii mwaka 2010 na 2014 huku wakishindwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo mwaka 2018 licha ya kufuzu, Hivo Lewandowski na wenzake wanataka kufuta makosa yao kwenye michuano iliyopita huku ndoto ya staa huyo pia ni kuifungia nchi yake bao kwenye michuano hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa