Golikipa wa timu ya taifa ya Costa Rica na klabu ya PSG Keylor Navas atakuwepo siku ya jumatano kuikabili timu ya taifa ya Hispania katika mchezo wa kwanza kundi E.

Golikipa huyo ambaye hajatumika kwa muda mrefu kwenye kikosi cha mwalimu Christopher Galtier kwasababu ya majeruhi na amekua akicheza golikipa wa kimataifa wa Italia Gigi Donarumma hivo kuibua mijadala huenda kipa huyo akakosekana Qatar.navasMeneja msaidizi wa kikosi cha Costa Rica Ronald Gomez amefunguka na kueleza golikipa huyo atakuwepo kwenye mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Uhispania siku ya jumatano kwenye mchezo wa kwanz awa kundi E.

Keylor Navas amekua akisumbuliwa na mgongo kwa muda lakini bwana Gomez anaeleza matatizo hayo yameshatatuliwa na golikipa huyo yuko tayari kuonesha ubora ambao amekua akiuonesha kila wakati analitumikia taifa hilo.navasNavas golikipa huyo wa zamani wa Real Madrid amekua akiitumikia timu ya taifa ya Costa Rica kwa kiwango cha juu huku ikiwa hii ni michuano yake ya tatu na taifa hilo kwani alianza mwaka 2014,2018 na mwaka huu 2022.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa