Baadhi ya mataifa mashuhuri Barani Ulaya yamepanga kugomea agizo la shirikisho la mpira duniani Fifa baada ya kupanga kuvaa vitambaa vya unahodha vyenye alama za upinde wakati huo Fifa imekataza.

Shrikisho la mpira wa miguu Fifa limetoa maelekezo kua timu zote hazitaruhusiwa kuvaa vitambaa vya unahodha vyenye alama ya upinde lakini baadhi ya mataifa yamepanga kukaidi amri hiyo na kuahidi wataendelea kuvaa kama ilivyokua awali.

Mkurugenzi wa soka kutoka nchini Denmark akifahamika kama Peter Moller yeye amesema nahodha wa timu yao Simon Kjaer ataendelea kuvaa kitambaaa chenye alama za upinde kama ambavyo wamekua wakivaa kwenye michuano ya Uefa Nations League.

Huku Mkurugenzi huyo wa michezo kutoka Denmark anaamini ataungwa mkono na mataifa mengine makubwa kutoka nchi za ulaya ili kukaidi agizo hilo lililotolewa na Fifa mapema wiki ikijaribu kutoka maelekezo ya vitambaa vitakavyovaliwa.

Fifa wao walikataza vitambaa hivo kwasababu nchi michuano inapofanyikia haifungamani wala kukubaliana na sera ambazo nchi za ulaya wanaziunga mkono kama mapenzi ya jinsia moja kitu ambacho hakikubaliki nchini Qatar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa