Potter Akanusha Aubameyang Kwenda Los Angels Galaxy kwa Mkopo

Kocha wa klabu ya Chelsea Graham Potter amekanusha mshambuliaji wake Pierre Aubameyang anakaribia kujiunga kwa mkopo na klabu ya Los Angels Galaxy ya nchini Marekani.

Taarifa za mwanzo zilieleza kua mshambuliaji huyo anajiandaa kujiunga na Los Angels Galaxy ya nchini Marekani kwa mkopo, Lakini kocha Potter amekanusha taarifa hizo na kusema taarifa hizo hazina ukweli wowte na Aubameyang ataendelea kusalia Chelsea.potterMshambuliaji Aubameyang amekua na kipindi kigumu ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kupata majeraha ya mara kwa mara, Vilevile kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Chelsea kitu ambacho kinaelzwa kumfanya mchezaji huyo kufikiria kutimka klabuni hapo.

Mshambuliaji Aubameyang ambaye alitoka klabu ya Barcelona na kujiunga na klabu ya Chelsea mwanzo wa msimu huu bado hajafanikiwa kuonesha makali yake ndani ya klabu hiyo, Lakini matumaini juu yanaonekana bado yapo na ndio sababu ya kuendelea kumshikilia mchezaji huyo.potterKocha Graham Potter amesisitiza kua Aubameyang anaendelea vizuri ndani ya klabu hiyo ana anafanya mazoezi ndani ya timu hiyo, Hivo suala la mshambuliaji huyo kujiunga na miamba ya soka nchini Marekani halipo kwasasa kama ambavyo iliripotiwa hapo awali.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.