Gabriel Jesus Afanya Mazoezi na Wenzake

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Brazil Gabriel Jesus ameanza kufanya mazoezi na wenzake kuelekea mchezo wa kombe la Europa dhidi ya klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno Alhamisi hii.

Mshambuliaji Gabriel Jesus amekaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu sasa tangu alipoumia kwenye michuano ya kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Brazil, Lakini amefanikiwa kupona majeraha ambayo yalikua yakimsumbua hivo anaweza kuanzia nje kwenye mchezo wa Europa Alhamisi hii.gabriel jesusGabriel Jesus alifanyiwa upasuaji wa goti mapema Novemba baada ya kuumia akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia, Mshambuliaji huyo alikua na msaada mkubwa ndani ya klabu ya Arsenal tangu atue klabuni hapo tangu atue akitokea klabu ya Manchester City msimu uliomalizika.

Kocha Mikel Arteta amemzungumzia mchezaji huyo na kusema kua hayupo mbali kurejea baada ya kushinda katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza jumamosi dhidi ya Bournamouth, Hivo ni wazi kua mshambuliaji hayupo mbali kurejea katika timu hiyo huku akiw atayari ameanza mazoezi na wenzake.gabriel jesusGabriel Jesus anarejea ndani ya timu hiyo na kuikuta ikiendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya alama tano kama mabvyo aliiacha, Kumekua na pengo la mshambuliaji huyo ndani ya klabu ya Arsenal baada ya kuumia kwake lakini haikufanya klabu hiyo iache kupata matokeo mazuri na kushinda michezo yake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.