Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen amerejea rasmi ndani ya klabu hiyo baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Eriksen amekaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu kwani kiungo huyo ameumia tangu mwezi wa kwanza katika mchezo wa kombe la Fa dhidi ya Reading, Kitu kilichomfanya mchezaji huyo kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu lakini hatimae mchezaji huyo amerejea rasmi kwenye mazoezi ya timu hiyo na timu ya kwanza.
Kiungo huyo aliripotiwa kurudi kwenye timu hiyo wiki moja nyuma lakini hakua ameweza kufanya mazoezi na wenzake, Siku ya jana mchezaji huyo ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wa klabu hiyo hivo kuonesha ni rasmi sasa amerejea ndani ya klabu hiyo.
Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuhusu mchezo wa kesho dhidi ya Everton na kusema habari nzuri ni kua kiungo Eriksen amerejea kwenye kikosi na atakuwepo kwenye sehemu ya kikosi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Everton.
Christian Eriksen amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya Manchester United na kua msaada mkubwa sana ndani ya timu hiyo kabla ya kupata majeraha, Hivo kurejea tena kwa kiungo huyo inakua ni habari njema kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kiwango ambacho alikua anakionesha kiungo huyo.

