Guardiola: Haaland Atakuwepo dhidi ya Southampton

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kua mshambuliaji wake matata Earling Haaland atakuepo kwenye mchezo wao wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Southampton hapo kesho.

Kocha Pep Guardiola amethibitisha hilo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao dhidi ya Southampton ikiwa ni baada ya kukosekana katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi iliyomalizika dhidi ya klabu ya Liverpool ambapo walipata ushindi wa 4-1.GuardiolaEarling Haaland alikosekana katika mchezo ambao Manchester City ilipata matokeo ya ushindi dhidi ya Liverpool, Lakini mchezaji huyo ni wazi wikiendi hii atakuepo uwanjani kuhakikisha anaiwakilisha klabu yake kuelekea wiki ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Kocha Guardiola alisema “Amekua akifanya mazoezi vizuri siku mbili zilizopita” Hii ni kauli ya kocha huyo ambaye ameweka wazi kua mchezaji huyo atakua sehemu ya kikosi kesho dhidi ya klabu ya Southampton hivo nguvu imeongezeka kikosini kwa mara nyingine baada ya kurejea kwa mshambuliaji huyo.GuardiolaKlabu ya Manchester City kesho wanaweza kupata nafasi ya kupunguza pengo la alama baina yao na vinara klabu ya Arsenal kwani wana uwezo wa kupunguza pengo la alama mpaka kufikia tano, Ambapo Arsenal watakua wanacheza siku ya jumapili dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield.

Kocha Guardiola vilevile ameiongelea klabu ya Southampton ambao ndio wapinzani wao siku ya kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza,Akisema klabu hiyo ni moja ya timu ngumu ambazo amekua akikutana nazo na mara kwa mara wamekua wakicheza vizuri dhidi yao hivo anatarajia mchezo wenye ushindani mkubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.