Benjamin Sesko Kuongeza Miaka Mitano Rb Leipzig
Makala iliyopita
Barella Kuongeza Mkataba Inter Milan
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Slovenia amekua akifuatiliwa na vilabu kadhaa ambapo klabu ambayo ilikua ikimfuatilia zaidi siku za hivi karibuni ni klabu ya Arsenal, Hivo mchezaji huyo kuongeza mkataba mpya ndani ya Rb Leipzig sio habari nzuri kwa washika mitutu hao kutoka jiji la London.
Klabu ya Rb Leipzig imekua ikisifika kwa kutoa wachezaji wenye ubora mkubwa miaka ya hivi karibuni na hii inatokana na ubora wao kutafuta vipaji barani ulaya na nje ya bara la ulaya, Jambo ambalo limefanya kupata vipaji vingi kama vya mshambuliaji Benjamin Sesko ambaye atasaini mkataba wake mpya kesho ndani ya timu hiyo.