Kibabage Arejesha Mabegi Singida Black Stars

Aliyekuwa beki wa kushoto wa Yanga SC, Nickson Kibabage tayari amejiunga na Singida Black Stars kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya mara baada ya kuachana na mabingwa hao wa ligi kuu msimu uliopita.

Beki huyo alikuwa katika kikosi cha Yanga SC msimu wa 2024/25. Akifanikiwa kutwaa taji la ligi, kombe la CRDB Confederation Cup, na ngao ya jamii kwa msimu wa 24/25 chini ya Kocha Mkuu Miloud Hamdi ambaye kwa sasa hayupo ndani ya kikosi hicho ambacho kwa sasa kinanolewa na Romain Folz ambaye ni raia wa Ufaransa na kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya msimu mpya 2025/26.

Kibabage Arejesha Mabegi Singida Black Stars

Inaelezwa kuwa taratibu zote za uhamisho wa beki huyo aliyempisha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyejiunga na Yanga SC kwa mkataba wa miaka miwili zimekamilika hivyo Kibabage kuelekea msimu ujao atakuwa kwenye uzi wa wababe hao wa Singida.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Rekodi za Kibabage ndani ya Yanga kwa msimu uliopita hazikuwa nzuri sana kwani hakufanikiwa kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi na ndani ya michezo yote 30 ya ligi kuu alipata nafasi ya kucheza jumla ya mechi 12 pekee. Katika mechi hizo 12 alicheza jumla ya dakika 889, hivyo huenda hii ikawa ni moja ya sababu ya kwanini ameamua kwenda kutafuta changamoto mpya kwa msimu ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kibabage Arejesha Mabegi Singida Black Stars

Ikumbukwe kwamba Kibabage anarejea Singida Black Stars ambayo ni timu  aliyokuwa akiitumikia kabla ya kujiunga na Yanga SC.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.