Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema maandalizi ya kuelekea mashindano ya Mataifa Arika AFCON 2027 yanaendelea vizuri huku kazi za kuboresha miundombinu ya michezo zikiendelea katika viwanja mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 6, 2026 na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamis Mwinjuma, baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati katika Benjamin Mkapa Stadium na Uhuru Stadium.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mhe. Mwinjuma amesema Serikali inaendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo ili kuhakikisha Tanzania inakuwa tayari kwa mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Ameeleza kuwa mashindano ya AFCON 2027 yatafanyika kwa ushirikiano wa nchi tatu za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda kupitia zabuni ya pamoja inayojulikana kama Pamoja.
Kwa mujibu wa Serikali, mashindano hayo yanatarajiwa kuleta fursa kubwa katika maendeleo ya michezo, uchumi pamoja na utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Serikali pia imesisitiza kuwa ina dhamira ya kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika kwa wakati ili Tanzania iwe mwenyeji bora wa mashindano hayo ya kihistoria barani Afrika.


