Elie Mpanzu Asaini Mkataba Mpya wa Miaka Miwili Kuendelea Kubaki Simba SC

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Elie Mpanzu Kibisawala, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake Msimbazi.

Elie Mpanzu Asaini Mkataba Mpya wa Miaka Miwili Kuendelea Kubaki Simba SCHatua hiyo inakuja wakati mkataba wake wa awali ulikuwa ukielekea ukingoni, huku uongozi wa klabu ukionesha dhamira ya kuendelea kuboresha kikosi chao kwa ajili ya mafanikio ya baadaye.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kupitia taarifa iliyotolewa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Simba, klabu hiyo ilithibitisha rasmi kufikiwa kwa makubaliano hayo mapya, huku ikieleza kuwa nyota huyo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ataendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho kwa misimu miwili ijayo.

Katika taarifa hiyo, Simba pia ilitoa pongezi maalum kwa Rais wao wa heshima, Mohammed Dewji, maarufu kama Mo, kwa juhudi zake kubwa zilizowezesha kufanikisha zoezi la kumbakisha mchezaji huyo muhimu ndani ya klabu. Uongozi umeeleza kuwa mchango wake umekuwa chachu ya mafanikio ya timu hiyo ndani na nje ya uwanja.

Elie Mpanzu Asaini Mkataba Mpya wa Miaka Miwili Kuendelea Kubaki Simba SCElie Mpanzu, ambaye ni kiungo mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kushambulia na kusaidia safu ya ushambuliaji, ameonyesha kiwango cha kuvutia tangu ajiunge na Simba, jambo lililowafanya viongozi wa klabu kuona umuhimu wa kuendelea kuwa naye kikosini, wakitarajia kuona mchango mkubwa zaidi kutoka kwa mchezaji huyo katika misimu ijayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.