Mwamuzi wa Ujerumani, Felix Zwayer, ambaye aliwahi kutiwa hatiani kwa tuhuma za upangaji matokeo mwaka 2005, ameteuliwa kuamua mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya Denmark na North Macedonia utakaopigwa Alhamisi usiku katika Uwanja wa Parken.
Zwayer mwenye umri wa miaka 43 aliwahi kufungiwa kwa miezi sita na German Football Association mwaka 2005 kufuatia kuhusika kwake katika kashfa ya upangaji matokeo. Adhabu hiyo ilitokana na kazi yake kama mwamuzi msaidizi chini ya Robert Hoyzer, ambaye alikutwa na hatia ya kupokea rushwa ili kupanga matokeo ya michezo kadhaa ya Ligi Daraja la Pili nchini Ujerumani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa taarifa, Zwayer alidaiwa kupokea euro 300 kabla ya mchezo ulioshirikisha timu ya Wuppertaler SV, hata hivyo baadaye alichukua hatua ya kuripoti vitendo hivyo kwa shirikisho la soka la Ujerumani, akisaidiwa na waamuzi wengine watatu waliothibitisha madai yake dhidi ya Hoyzer.
Kashfa hiyo haikujulikana kwa umma hadi mwaka 2014 baada ya gazeti la Ujerumani Die Zeit kuchapisha uchunguzi maalum ulioitwa “The Zwayer File”, ulioweka wazi historia ya adhabu hiyo. Wakati huo huo, Hoyzer alifungiwa maisha yote kujihusisha na soka.
Mwaka 2021, kurejea kwa Zwayer katika uamuzi wa mechi kubwa kulizua mjadala, ambapo kiungo wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham, alimkosoa wazi baada ya mchezo dhidi ya Bayern Munich akisema: “Unampa mwamuzi aliyewahi kupanga matokeo mechi kubwa zaidi nchini Ujerumani, unatarajia nini?”
Hata hivyo, Zwayer anaendelea kuaminiwa na mamlaka za soka, ambapo ni siku tano tu zimepita tangu aliposimamia mchezo mwingine muhimu nchini Denmark kati ya FC Midtjylland na Nottingham Forest katika michuano ya Europa League.

