Timu ya taifa ya Mali imeingia kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Urusi utakaopigwa Machi 31 katika dimba la Gazprom Arena.
Kikosi hicho kinaingia kwenye mchezo huo kikiwa na sura mpya kufuatia kuachwa kwa baadhi ya nyota wake muhimu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Miongoni mwa majina makubwa yaliyokosekana kwenye kikosi hicho ni Amadou Haidara, Lassine Sinayoko, Yves Bissouma pamoja na Sikou Niakate na goli kipa wao namba moja Djigui Diara, huku sababu zikitajwa kuwa ni mchanganyiko wa majeraha, mapumziko na maamuzi ya benchi la ufundi.
Kutokuwepo kwa wachezaji hao kunaashiria wazi mabadiliko makubwa ndani ya kikosi cha Mali, ambacho kinaonekana kuanza mchakato wa kujenga upya timu yenye ushindani zaidi kuelekea mashindano yajayo ya kimataifa.
Hali hiyo imefungua milango kwa wachezaji chipukizi kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wao na kujihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha taifa, jambo linalotarajiwa kuongeza ushindani wa ndani ya timu

