Taifa Stars Yaanza Vibaya FIFA Series, Gamond Aomba Radhi Baada ya Matokeo

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Miguel Gamondi, amewaomba radhi Watanzania kufuatia kipigo cha bao 1-0 walichopata dhidi ya timu ya taifa Liechtenstein team katika mchezo wa kwanza wa michuano ya FIFA Series.

Taifa Stars Yaanza Vibaya FIFA Series, Gamond Aomba Radhi Baada ya Matokeo  Gamondi amekiri kuwa matokeo hayo hayakutarajiwa na hayalingani na maandalizi pamoja na matarajio ya mashabiki wa soka nchini.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Akizungumza baada ya mchezo huo ulio pigwa kwenye dimba la Kigali Pele stadium nchini Rwanda, Gamondi alieleza kuwa timu ilifanya makosa kadhaa ya kiufundi na kushindwa kutumia nafasi walizozipata, jambo lililowagharimu na hatimaye kupoteza mchezo huo muhimu.

Taifa Stars Yaanza Vibaya FIFA Series, Gamond Aomba Radhi Baada ya Matokeo  Hata hivyo kocha Miguel Gamond alisisitiza kuwa benchi la ufundi litafanya tathmini ya kina ili kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza.

Kwa upande wake,kiungo mshambuliaji wa Taifa Stars, Novatus Miroshi, amesema kufungwa kwao ni aibu kubwa kwa timu hiyo kutokana na kuwadharau wapinzani wao.Miroshi alikiri kuwa walishindwa kuingia uwanjani wakiwa na umakini wa kutosha, hali iliyochangia kupoteza mchezo huo.

Taifa Stars Yaanza Vibaya FIFA Series, Gamond Aomba Radhi Baada ya Matokeo  Ameongeza kuwa wachezaji wanatambua uzito wa matokeo hayo na wamejipanga kurejea uwanjani kwa ajili ya mazoezi maalum ili kurekebisha makosa yao kabla ya michezo ijayo ya mashindano hayo. Pia aliahidi kuwa wataonyesha mabadiliko makubwa katika mechi zijazo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.