Kikosi cha Taifa Stars leo kinaanza rasmi kampeni ya michuano ya FIFA Series 2026 kwa kukabiliana na Liechtenstein katika Uwanja wa Kigali Pele, nchini Rwanda, mchezo unaotarajiwa kuanza saa 11:30 jioni.
Stars inaingia kwenye mchezo huo ikiwa inashikilia nafasi ya 110 kwenye viwango vya ubora vya FIFA, ikilinganishwa na wapinzani wao Liechtenstein waliopo nafasi ya 205, hali inayowapa Watanzania matumaini ya kufanya vizuri.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha mkuu wa Taifa Stars Miguel Gamondi amesema malengo yake juu ya kukifundisha kikosi cha Taifa stars ni kutengeneza kikosi kilichobora na chenye Ushindani.
Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wa FIFA series 2026. Gamondi ameeleza kwamba ataenda kumiliki mpira na kucheza soka safi kwakuwa ndio falsafa zake.
Aidha Gamondi amesisitiza kwamba hawezi kuahidi ushindi bali anaamini wanapomilikj mpira ndiyo watapata nafasi ya kutengeneza nafasi ma kushinda mchezo.
Naye Golikipa wa Timu ya Taifa ya Tanzania Aishi Manula amesema kucheza dhidi ya Timu za ulaya inawajenga wao kama wachezaji na pia ni fursa pia kwao kujitangaza katika mechi hizo ambazo wanaenda kucheza kuanzia hii leo.
Wameyasema hayo akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wa kesho wa FIFA SERIES 2026 utakaofanyika katika Jiji la Kigali Nchini Rwanda.

