Klabu ya Simba SC imefanikiwa kunasa saini ya winga mahiri Ramadhan Chobwedo kutoka TRA United, katika dili lililochukua sura mpya baada ya ushindani mkali kutoka kwa vigogo wengine wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Awali, Singida Black Stars walikuwa wa kwanza kufikia makubaliano ya kumpa mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili, lakini Chobwedo hakufunga mlango kwa ofa nyingine, akiendelea kusikiliza timu mbalimbali zilizokuwa zikimuwania.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Baadaye, Yanga SC waliingia rasmi kwenye kinyang’anyiro hicho kwa kumpa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya shilingi milioni 150, wakionekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kunasa saini yake.
Hata hivyo, mambo yalibadilika ghafla baada ya Simba SC kuingilia kati dili hilo na kutoa ofa nono zaidi ya mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi milioni 180, hali iliyomshawishi mchezaji huyo kujiunga na wekundu wa Msimbazi kuelekea msimu ujao.
Pamoja na usajili huo, bado kuna mjadala mkubwa kuhusu nafasi ya Chobwedo ndani ya kikosi cha Simba SC, ambacho tayari kina wachezaji wa nafasi ya winga wenye ushindani mkubwa akiwemo Anicet Oura, Libasse Gueye pamoja na Elie Mpanzu.
Baadhi ya wachambuzi wa soka wanaamini kuwa huenda mchezaji huyo akakosa muda wa kutosha wa kucheza kutokana na ushindani uliopo, jambo ambalo linaweza kumfanya akae benchi kwa muda mrefu au hata kutolewa kwa mkopo ili kupata nafasi ya kucheza zaidi.

