Golikipa wa Atletico Madrid, Jan Oblack amesaini mkataba mpya hadi mwaka 2023.
Nyota huyu raia wa Slovakia, alikuwa bado ana miaka miwili iliyosalia kumaliza mkataba wake wa awali. Oblack alijiunga na Atletico Madrid akitokea Benfica mwaka 2014 mwezi Julai huku akifanikiwa kuwa golikipa muhimu klabuni hapo kama mrithi wa Thibaut Courtois.
Mkataba mpya aliousaini nyota huyu unaripotiwa kuwa na dau la kununua mkataba wake kwa paundi milioni 100. Staa huyu anafurahia kusaini mkataba unaompa mda mwengine wa kudumu klabuni hapo.
Nyota huyu mwenye umri wa miaka 26 ameweza kuanza kwenye gemu zote 32 za klabu msimu huu.
“Ninafurahi sana kusaini mkataba mpya na kuwa hapa, nitaendelea kuzilinda rangi hizi kwa uwezo wangu wote na kuendelea kufanya bidii zaidi.” -Oblack
Atletico Madrid wanaipata sahihi hii wakiwa wamejiandaa kumpoteza Lucas Hernandez kwenda Bayern Munich mwisho wa msimu huu.

