Meneja wa Newcastle United, Rafael Benitez, anasema kuwa hataweza kujihakikishia kuendelea kuwepo klabuni Manchester United hadi atakapokuwa na uhakika juu ya mpango wa mda mrefu wa klabu hiyo.
Mkataba wa meneja huyu unaenda hadi mwisho wa msimu huu na hajataka kuweka wazi kama atasaini mkataba mwingine au lah, alijiunga na klabu hii mwaka 2016.
Hata hivyo, kuna tetesi kuwa meneja huyu anatarajiwa kuchukua kibarua cha Tuchel pale PSG ambaye amepoteza fainali za za Coupe de France dhidi ya Rennes.
Benitez anasema kuwa kila siku wanafanya mazungumzo na mkurugenzi wa klabu hiyo lakini kuna namna wanatakiwa kufikia muafaka kuona namna gani kila mtu anaweza kunufaika na makubaliano watakayofikia kwa kuwa kwa sasa wanamitazamo tofauti.


Issa
Aelew asielewe aondoke newcastle