Totenham Hotspurs wamekuwa wakitesa sana kwenye zao 4 walizocheza kwenye dimba lao jipya. Kwa mara ya kwanza, West Ham wameweza kuwatoa nishai baada ya kuwalaza watalamu wa soka wa Spurs bao 0-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani ambao hakuna klabu nyingine iliyofanikiwa kushinda.
West Ham wamecheza vizuri zaidi kipindi cha pili wakibamba ushindi huu kwa goli pekee la Michail Antonio dakika ya 67, ushindi huu mwembamba ndiyo uliowapa rekodi ya kihistoria. Kwa ujumla Spurs walionekana kumiliki zaidi mpira, lakini hiyo haijawasaidia kuzifika nyavu za wageni wao na kukubali kipigo.

Baada ya kupoteza gemu hii Spurs wanakuwa kwenye hatari ya kupoteza nafasi ya 3 dhidi ya Chelsea, kama Chelsea atafanikiwa kushindsa mechi dhidi ya United Jumatatu.
Spurs bado wana gemu ya dhidi ya Ajax Jumanne, itakuwa ni kibarua kikubwa kwao kukutana na vijana wa Ajax kwenye mzunguko wa kwanza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Wataalamu wanasema mpira una dunda, kama watatumia gemu ya leo kujiboresha kwa kurekebisha makosa yaliyoonekana leo bila watafanya vizuri. Lakini haitakuwa kazi rahisi kuchuana na vijana wa Ajax wakicheza soka kama la leo.


Povel
Gud news