Meneja wa Liverpool amekanusha kasheshe iliyopamba moto kabla ya gemu dhidi ya Huddersfield Town kuwa yeye na Mo Salah walitupiana maneno.
Klopp alishuhudia vyema vijana wake wakisakata kabumbu na kuwalaza 5-0 vijana wa mjini Huddersfield Ijumaa usiku wakipata nafasi ya kurejea kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza.
Liverpool walionekana mapema kuwa wao ndio wanaelekea kushinda gemu hiyo kwa sababu ya fomu mbaya waliyokuwa nayo Huddersfield Town msimu huu ambao wanajikuta wanashuka daraja.
Mo Salah ni moja kati ya mastaa waliokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye ushindi huo wa bao nyingi akiweka nyavuni magoli yake 2, pia Mane akichapa 2 na Naby Keita akiweka nyavuni goli la ufunguzi.

Hata hivyo meneja huyu akizungumzia ushindi walioupata amewapongeza vijana wake kwa kazi nzuri. Alipogusiwa kuhusu kutupiana manenao na Salah, akakanusha na kutupia lawama kwa mitandao ya kijamii kuwa ndiyo inayokuza mambo, hakukuwa na kitu kama hicho.
Klopp anasema wakati mwingine ni viuzuri kutoamini asilimia tatu ya maneno ya mtandaoni. Kwa sababu huwa yanapotosha uhalisia mara nyingi.
Liverpool wamerejea kileleni wakiwa na pointi 91, pointi 2 tu zaidi ya wapinzani wao wakubwa Manchester City ambao wanatetea taji la EPL, Man City wana safari ya kuelekea Burnley Jumapili tarehe 28. Wakifanikiwa kushinda gemu hiyo watamtangulia Man City na kitakachokuwa kimebaki ni kuombeana dua mbaya tu.


Amani
maneno ya mtandaoni. huwa yanapotosha uhalisia mara nyingi.