Nyota wa Inter Milan, Mauro Icardi amesisitiza kuwa anahitaji kusalia klabuni Inter Milani licha ya seke seke kuhusu kusepa kwa staa huyu. Nyota huyu, mshambuliaji anayetokea Argentina amechapisha katika ukurasa wake wa Insatagramu kuwa bado ana mapenzi makubwa na klabu hiyo.
Icardi ametumia ukurasa wake wa Instagramu kwenye kipengele cha stories kukanusha baadhi ya stori zilizohadithiwa na waandishi na vyombo mbalimbali juu ya yeye kuhama klabuni Inter Milan.
“Hivi karibuni tasnia ya habari imekuwa ikisema vitu ambavyo hata haviwakilishi mawazo wala nia yangu, ninataka kuwaarifu mashabiki wetu kuwa nimeiambia klabu mara kadhaa kuwa nia yangu ni kusalia hapa.
Kuanzia leo na kuendelea, hakutakuwa na kutoelewana kwa namna yoyote. Narudia tena, nimeshaiambia klabu kuhusu nia yangu ya kusalia kwa sababu Inter ni familia yangu. Nyakati zitaweka wazi nani alikuwa mkweli.”
Ikumbukwe nyot6a huyu alikuwa kwenye mgogoro na timu yake, mgogoro ambao ulitajwa kuchangiwa na mkewe kwa asilimia kubwa. Ipo wazi sasa staa hguyu anataka kusalia Inter Milan.


isha
Icard nenda tuu