Waliojijengea Umaarufu Aina Mbili

Katika mchezo wa soka kuna umaarufu wa aina mbili ambao lazima uwepo na huwa ni kitu cha kawaida sana kuwepo kwani ni jambo ambalo halizuiliki kabisa. Umaarufu huu upo ule ambao huwa unatokana na kazi nzuri inayofanywa na mchezaji na ule unaofanywa kwa mabaya.

Japo kuna mengine hutokea kama ajali pale wachezaji wanapojaribu kujenga aina fulani ya umaarufu ndani ya vikosi vyao na ulimwengu wa soka kwa ujumla kwani lazima kikosi kiwe na mtu wa aina yake ambaye wanasema uchizi wake husaidia timu iweze kucheza soka zuri au ubaya wake kuigharimu timu.

Japo utukutu wa aina hii ukizidi huwa na madhara ya aina mbili ndani ya kikosi na kwa mchezaji mwenyewe, yaani kumfanya mchezaji kupotea kabisa kwenye ramani ya soka na mara nyingine kuigharimu timu yake. Baadhi yao ni kama Baloteli ambaye ubora wake umeteketea.

Lakini wapo wale ambao mazingira ya mchezo huwajenga kuwa watukutu japo wao kwa asili yao ni wachezaji wazuri wenye uwezo wa kipekee sana ndani ya uwanja na hata kukosekana kwao ni athari sana. Leo tutakurudisha miaka ya nyuma ili kuwaangalia nyota hao.

O.J. Simpson, mkasa wake ulikuwa ni wa kushtua ulimwengu wa soka kutokana na kufanya mabaya ya kifamilia na kuandika historia mbovu sana akiwa kama mchezaji. Hili linatupeleka miaka ya 1994 ambapo mchezaji huyo alikabiliwa na kesi ya mauaji huku ikisemekana mkewe Nicole Brown Simpson na rafiki yake huyo mwanamke, Ronald Goldman walikutwa wakiwa wameuawa huko Marekani na sakata zima la mauaji hayo kuonekana lilikuwa chini ya mikono ya nyota huyo. Kutokana na kusota mahakamani sana alipotea kabisa kisoka.

Maradona, inakumbukwa miaka ya 1991 alipata kibano cha kutokujihusisha na masuala ya soka kwa miezi 15, hiyo ni baada ya kuonekana anajihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na kuongeza nguvu. Nyota huyu ni tunu kubwa na ya aina yake ndani ya taifa lake la Argentina na amekuwa na jina la pekee katika ulimwengu wa soka lakini alifanya kitendo ambacho sio cha kisoka. Mara nyingine alikuwa akionekana kumbi za starehe akipigana.

Zinedine Zidane, mchezaji aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mara tatu akiwa ndani ya historia ya akina Ronaldo na Messi. Ndani ya ligi alizopita ikuwemo Ligue 1 na La Liga aliacha ramani za kipekee sana ndani ya ulimwengu wa soka. Alifanya kitendo kisicho cha kisoka mbele ya nyota mwenzake na raia wa Italia, Marco Materazzi kwenye mchezo wa kombe la dunia kitu kilichomfanya kutolewa uwanjani na kuigharimu timu yake na yeye kumaliza soka lake katika hali isiyokuwa ya kiuungwana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.