Bilionea Muitalia, Rocco Commisso ni mmiliki mpya wa klabu ya Fiorentina. Imethibitishwa kuwa tajiri huyu ameinunua klabu hii inayoripotiwa kuwa na thamani kati ya paundi milioni 160 na 170.
Tajiri huyu anatajwa kuwa amekuwa akifuatilia didli la kuimiliki klabu hii ya Fiorentina kwa karibia miaka mitatu sasa. Kabla ya kuinunua klabu hii, tajiri huyu alikuwa ni shabiki mkubwa soka la Italia mwenye ndoto ya kuwa mmiliki.
“Nimekuwa shabiki wa soka la Italia na hakuna maneno yanayotosha kuelezea heshima kubwa niliyopata kwa fursa hii ya kuchangia kuuandika ukurasa mpya wa historia ya klabu kubwa kama Fiorentina.” -Rocco Commisso
Commisso ni tajiri anayemiliki kampuni ya utangazaji (TV Company) ambayo ni ya 5 kwa ukubwa nchini marekani. Pia ni mmiliki wa timu nyingine ya soka ya New York Cosmos.
Bosi huyu alizaliwa Italia shemu inayofahamika Calabria na kuhamia nchini Marekani. Yupo kwenye orodha ya watu 500 matajiri ya jarida la Fobres. Pia alijaribu kuinunua klabu ya Inter Milan, dili ambalo lilibuma.


Povel tz
Habar njema
Furahav
Yuko vizuri bosi.
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri boss