Brighton Atawapiku Wenzake kwa Samatta?

Klabu za Ligi Kuu ya Uingereza -Premier League zinamfukuzia kwa kasi nyota wa Genk, ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania -Taifa Stars. Brighton anafukuzana na wenzake kumnasa staa huyu.

Samatta, maarufu zaidi kama ‘Samagoal’ kule Ubelgiji amewavutia klabu kadhaa za Ulaya na yeye akiwa na ndoto kubwa ya kuingia Ligi ya Primia; Siku kadhaa zilizopita staa huyu amethibitisha kuwa ana uwezo wa kuvivaa viatu vya Lomelu Lukaku pale Man United.

Brighton anaungana na klabu za Aston Villa, Leicester City, Burnley na Watford wote kutoka EPL wakiisaka sahihi yake. Thamani ya nyota huyu kwa sasa inatajwa kuwa ni paundi milioni 12.

Nyota huyu mkataba wake wa sasa na KRC Genk bado mwaka mmoja. Amefanya vyema katika ligi ya Ubelgiji kwa kumaliza msimu kama kinara wa magoli.

Samatta anasema klabu ya Brighton imekuwa ikimfuatilia kwa mda mrefu, mawasiliano hayakukatika kati ya wakala wake na klabu hiyo. Samataa anajona nje ya KRC Genk, ana matumaini makubwa kuwa atakuwa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Sio klabu za Uingereza pekee zinamfukuzia nyota huyu, klabu za Roma kutoka Italia na Lyon kutoka Ufaransa pia zinamtamani staa huyu. Tutarajie kumuona kwenye EPL msimu ujao mipango ikimuendea sawa staa huyu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.