Wachezaji Bora Afrika

Kuna idadi kubwa sana ya wachezaji wa Kiafrika ambao wanaheshimika kwa kiwango kikubwa ndani ya mataifa yao kwa mafanikio makubwa waliyoyapata na kusaidia pia ndani ya mataifa yao kuweza kufikia hatua fulani kwenye michuano mbalimbali mikubwa. Mbali na hilo, heshima hiyo wameipata kutokana na uwezo wao.

Vitu vinavyotambulisha ubora wao na kuwaacha wengine ni suala zima la ujuzi ikiwemo kasi na uwezo wa kuuchezea mpira, takwimu zao katika klabu na ngazi ya timu ya taifa, mataji yao na makombe waliyoshinda na klabu na pia, mataifa na mwisho, ni mafanikio yao kwenye soka kwa ujumla. Baadhi ya nyota hao ni:

George Weah (Liberia), alianza kujihusisha na soka alipokuwa na miaka 15 na baada ya miaka saba alipata nafasi ya kuitwa katika timu ya taifa. Kama ilivyo kawaida ya wachezaji wa ukanda huo, akafanikiwa kwenda Ufaransa ambako aliendelea kujihusisha na soka. Mwaka 1994 alikusanya tuzo zikiwemo mchezaji bora wa Kiafrika wa mwaka, mchezaji bora wa mwaka kwa Ulaya na mchezaji bora wa FIFA.

Augustine Azuka “Jay-Jay” Okocha (Nigeria), jina lenye heshima kubwa sana ndani ya ulimwengu wa soka duniani kote. Akiweza kutwaa mataji nchini humo kama mchezaji bora kwa miaka ya 1995, 1997, 2000, 2002, 2003, 2004, na 2005. Katika maisha yake ya soka akifanikiwa kuzichezea klabu za Eintracht Frankfurt, Fenerbahce, Paris Saint-Germain, the Bolton Wanderers na Hull City kwa mafanikio makubwa sana.

Hossam Hassan Hussein (Misri), mshambuliaji hatari sana ndani ya kikosi cha timu hiyo mwenye historia ya kipekee sana ndani ya taifa hilo. Uwezo wake na historia aliyoiweka ambayo hadi sasa bado haijaweza kufikiwa, akiweza kufunga magoli 70 kwenye mechi 169 alizocheza ndani ya Misri.

Yaya Touré, wengi walimbatiza kwa jina la ‘treni mtu’ kutokana na uwezo wake wa kunyumbulika akiwa uwanjani. Alistaafu kuchezea timu ya taifa mwaka 2015 lakini alirudi kuipa tafu timu mwaka 2017 akitaka kuivusha iweze kushiriki kombe la dunia japo hawakufanikiwa mbele ya Morocco. Amechukua tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara 4 na bado anacheza soka mpaka sasa.

Nyota wengine wanaokaa katika takwimu hizi ni:  Roger Milla (Cameroon), Rashidi Yekini (Nigeria), Didier Drogba (Ivory Coast), Samuel Eto’o (Caneroon), Nwankwo Kanu (Nigeria), Abedi ‘Pele’ Ayew (Ghana). Hawa wanaongoza jopo la wachezaji ambao kwa hakika wameacha alama kubwa ambayo wengine waliopo wanafuata nyayo zao kutokana na uwezo wao na aina ya safari waliyoipitia hadi walipofikia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.