Kikosi Kipya cha Stars

Tunaelekeza jicho letu kwenye michuano ya mataifa ya Afrika [AFCON] ambapo timu ya taifa ya Tanzania inashiriki ndani ya michuano hiyo kwa mwaka huu baada ya kupata nafasi ya kufuzu ikiwa kwao ni kama historia kubwa sana baada ya kuweza kufikia hatua ambayo kwa miaka mingi sana wamekuwa wakiitamani waweze kuifikia.

Kwa awamu hii wamepata nafasi hiyo baada ya kuonesha kiwango cha aina yake ili waweze kuiwakilisha nchi yao kwa nafasi kubwa. Ni jambo la kipekee na lenye upinzani sana kuwa ndani ya michuano hiyo ambayo kama taifa wana nia ya kusonga mbele pamoja na kukaa kwenye kundi ambalo lina ushindani mkubwa.

Huku kikosi cha taifa kikiwa Misri kuendelea kujifua katika kipindi hiki wapo kwenye hatua nzito sana ya kurejesha heshima ya miaka mingi sana. Kibarua ambacho kwa sasa kipo mikononi mwa wachezaji na kocha ambaye dhamana nzima ya taifa ipo mikononi mwake kwa sasa.

Hadi sasa kocha wa kikosi hicho amepata majina yake 23 ambayo yatachukua nafasi ya kubeba dhamana ya kikosi kizima kwenye michuano hiyo. Baada ya kuwa na kipindi kizito cha kupembua majina ya wachezaji ambao wangesalia ndani ya kikosi ambacho ni ile idadi inayotakiwa basi amefanikiwa kuyapata majina hayo sasa.

Baadhi ya nyota wakosa nafasi ya kusalia ndani ya kikosi cha Amunike ambaye ndiye anakiangalia kikosi hicho, kuna upekee kwa sababu anaondoa wachezaji bila kuangalia jina la nyota ila kupata mahitaji ya kimfumo zaidi na mafanikio kama taifa ili kupunguza uteja uliopo.

Abdi Banda anayekipiga katika klabu ya Baroka ameachwa nje ya kikosi cha watu 23 huku kila mtu akiwa na neno juu ya kutemwa kwa nyota huyo ambaye wengi wanaamini ana uwezo mkubwa sana wa kuweza kuisadia timu yake kuweza kusonga mbele kwenye michuano hiyo huko Misri.

Shiza Kichuya anayekipiga katika klabu ya Pharco huko huko Misri naye hajapata nafasi ya kumshawishi mwalimu ili aweze kumpa nafasi ya kuonesha uwezo wake ndani ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Mbali na hao wapo wengine kama vile David Mwantika kutoka Azam, Shaban Chilunda kutoka Tenerife na Kevin John kutoka timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 [U17]. Hao wameachwa katika kikosi cha mwisho ambacho pia leo kinategemewa kucheza mchezo wa kirafiki na Misri.

Makala iliyopita

4 Komentara

    Kikosi kimetulia

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.