Baada ya kuipa ubingwa wa UEFA Nations League, nyota wa taifa la Ureno ambaye amekuwa akivunja rekodi nyingi sana ndani ya taifa hilo ameweza kwa awamu nyingine kurudisha kombe hilo kwa mashabiki wa taifa hilo akiwa na nia ya kuwapa furaha ya kudumu maShabiki wake na raia wa taifa lake.
Katika kampeni nzima za kufika kunyanyua kombe hilo nyota huyo amecheza nafasi kubwa sana na ya pekee hadi kukifanya kikosi hicho kuonekana cha pekee na chenye ushindani wa aina yake duniani. Ikumbukwe uwepo wa nyota huyo ndani ya kikosi hicho mara nyingi huwa na chachu nzima ya ushindani.
Kwa sasa Ureno wameanza kurudi katika ramani ya soka na hata kama Ronaldo ataacha kucheza ndani ya kikosi hicho ni jambo lisilopingika kwamba atakuwa amekiacha kikosi katika mikono salama kabisa ya watu kama Bernado Silva ambao kazi yao wakiwa uwanjani sio ya kubahatisha na wana karama pekee ya soka.
Kwa uhakika wengi waliona kama kigezo cha umri kingepunguza sana uwezo wa nyota huyo lakini mambo yamekuwa tofauti sana amekuwa aina ya watu ambao tuseme watastaafu na mpira wao huku historia nyingine zikiwa ngumu sana kufikiwa na baadhi ya watu ambao wapo katika soka leo.
Pamoja na nafasi yake kama mchezaji pia amekuwa mhamasishaji mkubwa sana wa kikosi chao hicho ambacho kwao mafanikio yamekuwa jambo la kawaida. Vijana wengi wanapambana kufuata nyayo zake ndani ya maisha yake halisi ya soka na hata nje ya soka kwani ni aina ya watu ambao wanaelezeka.
Baada ya ushindi wa taji hilo sasa tuzo kubwa yenye heshima yaani Ballon d’Or inaonekana kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na mafanikio ambayo kila nyota ameyafikia kwa msimu huu. Kuanzia mashindano ya muda mrefu kati ya Messi na Ronaldo wakiwa na vikombe vizito ndani ya msimu na rekodi kadhaa.
Pia, wengine kama Salah, Van Dijk, Bernado Silva hakika kuna ushindani mkubwa sana wa nani hasa atakuwa amewazidi wenzake kutwaa tuzo hiyo. Ni imani yangu kwamba tuzo hiyo kwa msimu huu itakuwa na changamoto sana na wengi watakasirishwa sana na maamuzi yatakayotoka kwa mshindi maana bado kuna rekodi nyingi sana zimewekwa na wachezaji hao.
Hadi sasa ameshinda mataji matatu likiwemo la ligi, Italian Supercup na hili la sasa, UEFA Nations Cup. Hiyo tayari ni tiketi kubwa sana kwake na inampa heshima na nafasi kubwa sana kushindana na wengine kwenye nafasi hizo za kuwania tuzo hiyo.


Njiku
Nyota huyo was ureno yupo juu sanaa anafanya vizuri sanaa
Povel
Cr7 yupo vzr sana