Pereira Aongezewa Ulaji

Nyota wa klabu ya Manchester United ameaminiwa na kuongezewa mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo ya Manchester United ambako atapewa mkataba wa kusalia hapo kwa miaka minne zaidi baada ya kumvutia mwalimu na kuona kwamba ni aina ya wachezaji wenye matunda ndani ya klabu hiyo.

Ole Gunnar Solskjaer ndiye aliyetamani na kutaka klabu kumuongezea muda mchezaji huyo aendelee kusalia baada ya kuamini kwamba uwezo wake ni mkubwa na ni sehemu ya viungo watakaokuwa bora sana katika soka, hususan ndani ya klabu hiyo.

Pereira [23] kabla ya kushawishi kuitwa katika kikosi cha timu ya wakubwa ametumikia soka lake na kukuza zaidi uelewa wa soka nje ya klabu hiyo kwa kuchezea ligi nyingine kwa mkopo ikiwa ni pamoja na Granada na Valencia katika misimu ya 2016/17 na 17/18 ambako aliaminika na kurejeshwa upya kikosini.

Lakini msimu wa 2018/19 ulikuwa wa pekee sana kwa nyota huyo mbali na kwamba klabu haijaweza kufika inapopaswa kuwepo lakini kwake umekuwa msimu wa aina yake kutokana na kupata nafasi ya kuwakilisha kikosi hicho kwenye michuano mikubwa na hata ndani ya ligi kuu pia.

Baadhi ya mafanikio ambayo nyota huyo raia wa Brazil amepata ndani ya msimu huu ni yale aliyoyapata wakati wa mechi dhidi yao na Southampton ambapo goli lake dhidi ya klabu hiyo liliingia katika rekodi na kuwa goli bora la mwezi kwenye ligi. Hiyo kwake itabaki kuwa sehemu ya mafanikio.

Mkataba wa nyota huyo unafikia ukomo ndani ya msimu huu ulioisha 2018/19 lakini hawana wasiwasi wa kumpoteza nyota huyo na kama hivi tayari wanampa ulaji mwingine wa kuendelea kutumika hadi 2023 na hapo kwa umri wake atakuwa bado na uwezo wa kufanya makubwa zaidi.

Mbali na Pereira, pia, kama klabu tayari imesikiliza maombi ya mashabiki zake juu ya kumuacha Mata aendelee kukaa kikosini hapo maana anaaminika kwa kiwango chake na uwezo wa kubadili matokeo pale timu inapokuwa na nafasi ya kufanya hiyo. Mkataba wa Mata ulikuwa ukingoni lakini atapata ofa ya kusalia na miamba hao wa soka wa jiji la Manchester kwa kipindi kingine.

Kuna wengine ambao wameomba kutimka kikosini hapo wakiwemo wachezaji kama Ander Herrera na Antonio Valencia ili kupisha maingizo mengine katika zoezi zima la kujenga kikosi kipya chenye ushindani wa pekee zaidi.

3 Komentara

    Hongera kwake

    Jibu

    Hongera kwake

    Jibu

    Huu ndio wakati wake Pireirra

    Jibu

Acha ujumbe