Usajili wa msimu wa joto umepamba moto huku tukiwa ligi kuu ikiwa mbioni kuanza kwa msimu ujao. Hapa kuna orodha ya wachezaji wapya waliotimba Ligi Kuu ya Uingereza katika dirisha hili la usajili.
Tanguy Ndombele Ndani ya Spurs!
Tottenham Hotspurs wamemsainisha kiungo wa Ufaransa, Tanguy Ndombele mwenye miaka 22. Staa huyu ametokea klabu ya Lyon kwa dau la paundi milioni 58.8. Tanguy Ndombele amesaini mkataba hadi mwaka 2025 na dau lake linataratiwa kupanda hadi paundi milioni 70.
Aaron Wan-Bissaka kwa Mashetani Wekundu
Manchester United wamefankiwa kuinasa saini ya mchezaji Crystal Palace na Uingereza Aaron Wan-Bissaka kwa ada ya paundi milioni 50. Kinda huyu wa miaka 21 amesaini mkataba unaoenda kumlipa paundi 80,000 kwa wiki. Bosi Ole Gunnara anamtazama kinda huyu kama moja ya walinzi bora wanaochipukia katika soka la Ulaya.
Gabriel Martinelli atinga Arsenal
Washika mtutu, Arsenal wamekamilisa uhamisho wa nyota kijana wa Brazil Gabriel Martinelli mwenye umri wa miaka 18. Kinda huyu ni mshambuliaji na anaingia kwenye orodha ya wachezaji wa Arsenal kama mchezaji wa kwanza kusajiliwa msimu huu wa kiangazi.
Mateo Kovacic rasmi Chelsea
Mateo Kovacic alitumikia misimu miwili iliyopita klabuni Chelsea kwa mkopo akiwasaidia wakali hawa kutwaa ubingwa wa Europa. Kwa sasa Mateo Kovacic amesaini mkataba klabuni hapo kwa dau la paundi milioni 40. Chelsea walimsajili nyota huyu kwa mkopo na kwa sasa wamemsainisha kwa mkataba wa miaka mitano zaidi.
Chelsea wanatumikia kifungo cha kutosajili hadi mwaka 2020, Kovacic imekuwa rahisi kumsainisha mkataba kwa kuwa tayarei alishasajiliwa kwa mkopo.


Povel
Gud news
Furahav
Safi